Ubalozi mdogo wa China huko Kota Kinabalu nchini Malaysia umesema watalii 25 wa China wameokolewa baada ya meli waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye jimbo la Sabah, Borneo Kaskazini nchini humo.
Boti hiyo haikujulikana ilipo jana ikielekea Pulau Mengalum, kisiwa maarufu wa kitalii kutoka mji mkuu wa jimbo hilo Kota Kinabalu. Shirika la Utekelezaji Sheria Baharini la Malaysia limesema boti hiyo ilikuwa ikibeba watu 31 wakiwemo watalii 28 kutoka China.
Rais wa China Xi Jinping ametaka juhudi zaidi zifanyike za utafutaji na uokoaji wa watalii hao wa kichina.