Mashirika ya chakula na wakimbizi ya Umoja wa Mataifa yameeleza wasiwasi juu ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili wakimbizi wapatao milioni 2 katika nchi 10 barani Afrika.
Naibu msemaji wa Umoja huo Farhan Haq amesema, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Chakula la Dunia WFP na kamishna wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia mambo ya wakimbizi wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali mbaya ya wakimbizi.
Haq amesema idadi ya wakimbizi barani Afrika imeongezeka maradufu kutoka milioni 2.6 ya mwaka 2011 hadi kufikia karibu milioni 5 ya mwaka 2016.