Wafuasi wahafidhina wa rais mteule wa Marekani Donald Trump wamelalamikia uamuzi wa kiongozi huyo wa kutofuatilia uchunguzi mpya kuhusu kashfa ya barua pepe iliyomkabili mpinzani wake Hillary Clinton.
Bw Trump baadaye alifafanua na kusema hatua kama hiyo inaweza kuzua migawanyiko zaidi.
FBI walimuondolea Bi Clinton makosa lakini wafuasi wa Bw Trump walikuwa wakiimba "lock her up" (mfunge jela) kwenye mikutano yake ya kampeni.
Wafuasi wahafidhina sasa wanasema hatua hiyo ya Bw Trump ni "usaliti" na kwamba amevunja ahadi yake.
Tovuti ya Redstate.com imesema hatua ya Bw Trump kutomteua mwendesha mashtaka maalum wa kufuatilia tuhuma hizo dhidi ya Bi Clinton, kama alivyokuwa ameahidi, itafichua "ukweli kwamba yeye ni mtu aliyejidai kuwa wakati wa kampeni".
Tovuti ya mrengo wa kulia ya Breitbart News Network, moja ya tovuti za habari zinazomuunga mkono sana Bw Trump pia ilishutumu hatua hiyo na kusema ni "ahadi iliyovunjwa".
chanzo:bbc