Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemchagua gavana wa Carolina kusini, Nikki Haley, kuwa balozi mpya wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.
Hiyo imekuwa mojawepo ya nafasi ya juu zaidi katika utawala wake mpya, kumuendea mwanamke au mtu asiye mweupe.
Nikki Haley ambaye alimpinga Trump, wakati wa kampeini za kuwania kiti cha Urais ni Mwamerika wa pili mwenye asili ya Ki-ashia, kuchukua wadhfa wa Ugavana nchini Marekani.
chanzo:bbc