Watanzania watakiwa kuchangamkia ‘Black Friday’
Na Dotto Mwaibale
TUNAPOELEKEA mwisho wa mwaka wa 2016 huku sikukuu za krisimasi na Mwaka Mpya zikiwa zinakaribia, Watanzania wametakiwa kuchangamkia ofa za ‘Black Friday’ inayolenga kupunguza pakubwa bei ya kukaa kwenye hoteli nchini.
Rai hiyo imetolewa na kampuni inayotoa huduma za hoteli mtandaoni ya Jumia Travel ambapo inamuwezesha mtu kujionea hoteli mbalimbali, upatikanaji wa huduma, bei, mahali zilipo na pia fursa ya kuweza kulipia kabisa.
Mtandao huo umeingia makubaliano na hoteli kadhaa za Tanzania bara na visiwani Zanzibar katika kuhakikisha wateja wanaonja utamu wa huduma zao kwa punguzo kubwa ambalo limekuwa likiendelea kwa wiki mbili sasa na litafikia kilele mnamo Ijumaa tarehe 25 Novemba mwaka huu.
Akifafanua zaidi kuhusu siku hii ya Black Friday, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa hoteli ambazo zimetoa ofa hiyo ni pamoja na Africa House na Jaffreji House & Spa zilizoko katika Kisiwani Zanzibar pamoja na White Sands na Landmark Beach Resort & Conference Center zilizopo Tanzania Bara.
“Ninafahamu kuwa wengi wetu huwa tunatamani kutumia muda huu wa mapumziko katika sehemu nzuri yenye starehe zote tofauti na mazingira tuliyoyazoea. Hilo linawezakana kwani kupitia ushirikiano na hoteli tunazofanyakazi nazo tunawatangazia ofa ya punguzo kubwa la kwenda kujivinjari katika hoteli za nyota nne ambayo imeanza wiki iliyopita Novemba 14 na itadumu mpaka Novemba 25,” alifafanua.
“Kupitia ofa hii unaweza kuitumia pamoja na mpendwa wako, familia, ndugu, jamaa au marafiki. Kwa mfano, White Sands wanayo michezo ya kwenye maji, kituo cha kupiga mbizi chini ya maji na safari ya boti kwenda kisiwani. Tunawasihi watanzania kutumia fursa kama hizi ili kuweza kujionea huduma nzuri na hadhi ilizonazo hoteli za hapa nyumbani. Itakuwa ni jambo zuri sisi kwanza kuwa mabalozi wa vitu vyetu wenyewe na sio wageni wanaokuja kutembelea nchini.” Alimalizia Meneja huyo Mkazi wa Jumia Travel Tanzania
Kutokana na maendeleo ya teknolojia Jumia Travel (travel.jumia.com) inamuwezesha mteja kufanya huduma zote za hoteli kupitia programu inayoweza kupatikana kwenye kompyuta, tableti na simu. Hivyo basi kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa njia rahisi na uhakika bila ya kumlazimu mtu mpaka kutembelea hoteli anayoitaka moja kwa moja.
Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel (travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika ambao humruhusu mteja kupata bei nzuri za hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.
Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.
Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa).
Kabla ya mwezi Juni 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mnamo mwaka 2013 na Jumia huku ikiendeshwa kwa ushirikiano wa karibu na makampuni kama vile MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axa.